Rekodi hiyo, inayodaiwa kuwa na Rais wa Chuo Kikuu Santa Ono, inapendekeza kwamba vyuo vikuu vinashinikizwa kuweka kipaumbele kushughulikia chuki dhidi ya Uyahudi badala ya chuki dhidi ya Uislamu.
Chuo kikuu cha Michigan kimekuwa kitovu cha maandamano ya wanafunzi dhidi ya vita vya Israel dhidi ya Gaza. Muhula huu wa masika uliopita, wanafunzi waliweka kambi kwenye chuo kikuu, wakitaka chuo kikuu kujitenga na makampuni ya kibiashara yanayofungamana na Israel. Mwezi Mei, polisi wa kuzima ghasia waliwatimua waandamanaji wakitumia dawa ya pilipili na kuwakamata watu kadhaa.
Katika malalamiko yake, CAIR-MI imebaini kwamba utawala wa chuo kikuu umepuuza majaribio mengi ya kushughulikia maswala ya kubaguliwa Waislamu, Wapalestina, Waarabu, Waasia Kusini, na washirika wao wanaoiunga mkono Palestina.
Kundi hilo linataka uchunguzi ufanyike ili kubaini ikiwa chuo kikuu kinatii sheria ambayo inakataza ubaguzi kulingana na rangi, kaumu au asili ya kitaifa katika taasisi zinazofadhiliwa na serikali.
IQNA